Ruka hadi kwenye sehemu kuu

Mwongozo wa kupokea malipo kwenye akaunti yako ya benki ya US.

Unavyotakiwa kufanya na usivyotakiwa kufanya kwenye akaunti yako ya benki ya Marekani.

Aisha avatar
Imeandikwa na Aisha
Imesasishwa wiki hii

Hongera kwa kutengeneza akaunti yako mpya ya benki ya Marekani!! Tafadhali kumbuka yafuatayo:


  • Akaunti yako ya benki ya USD inaweza kupokea malipo kwa njia ya ACH. Aina ya akaunti yako ni Checking.

  • Kama anuani ya nyumbani ya US itahitajika, anuani ya benki inaweza tumika kama anuani ya mpokeaji.

  • Kiasi cha juu ya kupokea kwa kila muamala ni USD 20,000.

  • Kupokea malipo kwenye akaunti yako ya USD inaweza kuchukua kati ya siku 1 hadi 2.


Uhamishaji wa ACH

  • The Automatic Clearing House (ACH) ni mfumo wa kutuma malipo ya kielektroniki unaotumika US.Huu ni mfumo wa malipo ya ndani unaotumika na benki ndani ya Marekani.

  • Kupokea malipo kupitia ACH utakatwa ada ya 0.8% juku makato ya chini yakiwa ni USD 2 na ya juu ni USD 10.

  • Kupokea malipo kupitia ACH, tumia namba yako ya routing ya ACH.

Uhamishaji wa SWIFT

Uhamishaji wa SWIFT kwa sasa hausapotiwi.


Hatusapoti kupokea malipo kupitia Cryptocurrency, P2P, Ubashiri na malengo ya biashara za FOREX.

Unaweza kutazama ada zote za uwekaji fedha hapa.

Je, hili lilikuwa jibu la swali lako?