Ruka hadi kwenye sehemu kuu

Uthibitishaji wa KYC

Namna gani unaweza kumaliza KYC

Aisha avatar
Imeandikwa na Aisha
Imesasishwa wiki hii

KYC inaamaanisha mjue mteja wako.Ukifanikiwa kutengeneza akaunti yako na kuthibitisha barua pepe yako, Utatakiwa kuthibitisha KYC yako.Kabla hujafanya muamala wowote Grey, tunatarajia utakuwa umekamilisha KYC yako ili kuangalia uhalali na kuzuia ulaghai.

  • Ukishathibitisha barua pepe yako, utaulizwa unahitaji Grey kwa ajili gani, chagua kipi kinachokufaa halafu bofya “ Wasilisha

  • Utapelekwa kwenye ukurasa wako wa nyumbani.Bofya “ kamilisha utengenezaji wa akaunti

Hizi ni hatua unazotakiwa kufuata kukamilisha uthibitishaji wa KYC yako

HATUA YA 1

  • Jaza taarifa zako za anuani, jiji, msimbo wa posta, tarehe ya kuzaliwa na mwisho taarifa ya akaunti yako ya benki ya karibuni kisha bofya “ Endelea”

Taarifa ya akaunti yako ya benki inatakiwa iwe kwenye mfumo wa PDF, PNG au JPEG, Pia inatakiwa iwe chini ya MB3 na isiwe imezidi miezi mi 3.

HATUA YA 2

  • Lazima uthibitishe ikiwa wewe ni mtu aliyewekwa wazi kisiasa (PEP) au unahusiana na mtu aliyefichuliwa kisiasa. (PEP ni Mtu Binafsi ambaye amekabidhiwa majukumu mashuhuri ya umma, kwa mfano, wakuu wa nchi au serikali, wanasiasa waandamizi, wabunge, wakuu wa serikali, maafisa wa mahakama au jeshi, n.k.)

HATUA YA 3

Hatua hii ni ya kuthibitisha utambulisho wako

  • Bonyeza “ anza kuthibitisha utambulisha wako

  • Utatakiwa kupakia vifuatavyo

  1. Picha ya kitambulisho chako halisi kilichotolewa na serikali (Leseni ya udereva, kitambulisho cha utaifa, ama pasi ya kusafiria).Picha yako halisi ya kitambulisho itahitajika ✅, na sio nakala.❌

  2. Video fupi inayoonesha sura yako.

Ukimaliza kukamilisha mchakato huu, utapelekwa kwenye ukurasa uliokamilika.

Hati zako zitapitiwa na utapokea barua pepe ya ukamilisho pale tu utakapothibitishwa.Kumbuka hati zako zitapitiwa ndani ya dakicha chache au masaa 24.

Hati yako itakapothibitishwa, unaweza kutengeneza akaunti yako ya kigeni kwenye sarafu tunazosapoti kisha utaweza kufurahia safari yako ya kufanya miamala.

Mwongozo wa kukamilisha kuthibitisha utambulisho wako

  • Picha yako halisi ya kitambulisho✅ inahitajika na si nakala.❌

  • Kona zote za kitambulisho chako zinatakiwa kuonekana.

  • Maelezo yote kwenye kitambulisho chako yanapaswa kuwa wazi na yanayosomeka; habari yoyote inayokosekana hufanya hati kuwa batili; tafadhali zima mwanga wa tochi ili kuzuia mng’ao uliopitiliza wa hati.

  • Hati zilizohaririwa na kubadilishwa haziruhusiwi.

  • Mtu anayeonekana kwenye kitambulisho anatakiwa alingane pia na mtu anayeonekana kwenye video ya selfie.

  • Jina linaloonekana kwenye kitambulisho chako linatakiwa kufanana na jina lako la Grey.

  • Tafadhali chukua video kwenye chumba chenye mwanga wa kutosha na uhakikishe kuwa uso wako unaonekana vizuri kwenye video.

  • Hakikisha umezima VPN ama Router kabla hujaendelea

Kwa nini uthibitishaji wangu umefeli?

KYC inaweza kufeli kwa sababu mbalimbali, baadhi ya sababu zimeorodheshwa hapa.

Tafadhali fuata muongozo kama unavyoelekeza.

Ukihitaji msaada zaidi kuhusu uthibitishaji, tumia gumzo lililopo ndani ya program au barua pepe [email protected], timu yetu ya usaidizi itakujibu haraka iwezekanavyo.

Je, hili lilikuwa jibu la swali lako?