Ruka hadi kwenye sehemu kuu

Document verification Uthibitishaji wa hati

Namna ya kukamilisha uthibitishaji wa hati.

Aisha avatar
Imeandikwa na Aisha
Imesasishwa wiki hii

Ukikamilisha kutengeneza akaunti yako na kuthibitisha barua pepe, utahitaji kuthibitisha utambulisho wako. Kabla hujafanya muamala wowote Grey, tunatarajia ukamilishe KYC na uthibitishaji wa hati yako ili kuangalia dalili za ulaghai.

Huu ni mwongozo wa kukamilisha uthibitishaji wa hati yako

  • Ingia kwenye akaunti yako ukithibitisha barua pepe yako.

  • Kwenye ukurasa wako wa nyumbani, bofya “ kamilisha utengenezaji wa akaunti”.

  • Utapelekwa kwenye ukurasa wa kuthibitisha hati yako, hakikisha unafuata maelekezo yako.

Vidokezo vya uthibitishaji wa hati

  • Pakia kitambulisho chako halisi kilichotolewa na serikali ( leseni ya udereva, kitambulisho cha utaifa, ama pasi ya kusafiria). Picha ya kitambulisho chako halali kinahitajika ✅ na sio nakala.

  • Kona zako zote za kitambulisho lazima ziwe zinaonekana vizuri.

  • Maelezo yote kwenye kitambulisho chako yanapaswa kuwa wazi na yanayosomeka; taarifa yoyote inayokosekana inaifanya hati kuwa batili; zima mwanga wako wa tochi ili kuzuia mng’ao kwenye hati.

  • Hati zilizohaririwa na kubadilishwa hazitokubaliwa.

  • Taarifa za kwenye kitambulisho chako lazima ziendane na taarifa za kwenye akaunti yako ya Grey.

Hati tunazosapoti

Utatakiwa utupatie nakala halisi ya vifuatavyo:

  • Kitambulisho cha kupiga kura

  • Pasi ya kimataifa

  • Kitambulisho cha taifa

  • Leseni ya udereva

  • Kitambulisho cha mkazi

Mwongozo wa kupakia selfie

  • Mtu anayeonekana kwenye kitambulisho lazima alingane na anayeonekana kwenye selfie.

  • Chukua video sehemu yenye mwanga na hakikisha uso wako unaonekana vizuri kwenye video.

Ukimaliza mchakato huu utaelekezwa kwenye ukurasa wa ukamilisho.Hati zako zitapitiwa na utapokea barua pepe ya uthibitisho pale taarifa zako zitakapothibitishwa.

Kikawaida uthibitishaji unachukua muda gani?

Tafadhali kumbuka kuwa hati hukaguliwa ndani ya dakika chache hadi masaa 24.

Baada ya hili, Unaweza kutengeneza kadi yako ya akaunti ya mtandaoni kwenye sarafu tunazosapoti na kubadili fedha.

Je, hili lilikuwa jibu la swali lako?