Ruka hadi kwenye sehemu kuu

Uthibitishaji wa sababu mbili.

Weka uthibitishaji wa sababu mbili ili kuongeza nguzo ya ziada ya usalama na ulinzi.

Aisha avatar
Imeandikwa na Aisha
Ilisasishwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita

Uthibitishaji wa sababu mbili ni utaratibu nwa kiusalama ambapo mtumiaji anatumbia njia mbili za uthibitishaji ili kujihakiki.

Mara ningi huwa na nenosiri/Passcode kama sababu ya kwanza ya uthibitishaji, kisha tokeni ya usalama (OTP) ama sababu ya kibayometriki ( alama ya vidole au usoni).

Kuweka uthibitishaji wa sababu mbili kwenye akaunti yako.

  • Ingia kwenye akaunti yako aidha kwa kutumia tovuti au programu ya simu.

  • Kwenye programu ya simu, bofya “zaidi” na chagua uthibitishaji wa sababu mbili.

  • Kwenye tovuti, bonyeza mpangilio kuufikia ukurasa wa mpangilio.

  • Chagua namna unavyotaka kupokea msimbo wa uthibitishaji

Kutumia programu ya uthibitishaji

Kuruhusu uthibitishaji wa sababu mbili kwa kutumia programu ya uthibitishaji, unatakiwa upakue na kusanikisha programu kwenye simu yako.Program za uthibitishaji ni pamoja na Google authenticator au Duo, kati ya nyingine nyingi.

Chagua “programu ya uthibitishaji”.

Scan msimbo wa QR unaoonekana kwenye app yako ya uthibitishaji ama ingiza setup key.

Bonyeza “Inayofuata”

Bonyeza msimbo wa namba sita uliotengenezwa na programu ya uthibitishaji na bofya “Wezesha”

👍 Umefanikiwa kutengeneza uthibitishaji wa sababu mbili kwa kutumia app ya uthibitishaji.

Kwa kutumia chaguo la Whatsapp

kuruhusu uthibitishaji wa sababu mbili kwa njia hii, tafadhali bofya hapa.

Chaguo la SMS kwa sasa halipo.

Kwa usalama bora, tunashauri utumie programu ya uthibitishaji.

Je, hili lilikuwa jibu la swali lako?