Utengenezaji wa akaunti nyingi Huwa tunashauri kutokutengeneza akaunti nyingi kwa sababu hii inaweza kuripotiwa kama tabia ya ulaghai na inaweza kusababisha akaunti yako kuwekewa vikwazo.
Kama unahitaji kutengeneza akaunti mpya, tafadhali fuata hatua zifuatazo.
Futa akaunti za nyuma: Hakikisha numefuta akaunti zilizopita kabla ya kutengeneza akaunti mpya.
Subiri masaa 48: Ruhusu masaa 48 yapite kabla hujatengeneza akaunti mpya kuepuka changamoto.
Ufutaji wa akaunti.
Kama umedhamiria kufuta akaunti kutokana na taarifa zisizo sahihi, mabadiliko ya barua pepe ama tarehe ya kuzaliwa, hivi ndio vitu vya kuzingatia:
Ili kuzuia matatizo, epuka kufuta na kutengeneza akaunti mpya haraka.
Omba usaidizi na fuata maelekezo kwa umakini ili kutatua matatizo pasipo haja ya kufuta akaunti.
Kumbuka, unaweza kuwa na akaunti moja (1) pekee, na hauruhusiwi kuwa na akaunti nyingi. Kudumisha uadilifu wa akaunti ni muhimu kuzuia kuepuka akaunti yako kusimamishwa. Kama kufuta akaunti ndio njia yako ya mwisho, unaweza kuwasiliana na timu ya usaidizi kwa msaada.