USDC (USD coin) ni aina ya sarafu ya cryptocurrency ambayo inajulikana kama stablecoin ambayo inaungwa mkono na mali ya dola ya Kimarekani na imeainishwa kwa thamani ya dola ya Marekani.
Tunakubali kutuma malipo kutoka kwa salio la USD hadi kwa pochi ya USDC pekee.
Ufuatao ni mwongozo wa hatua kwa hatua wa kutuma USDC.
Ingia kwenye akaunti yako.
Ingia kwenye “ akaunti” kisha chagua salio la USD.
Bofya “ Tuma pesa “ kisha chagua “ Tuma kwa Crypto”
Jaza taarifa zote, kisha chagua mtandao sahihi; "Solana (SOL) chain au Binance Smart Chain (BEP-20)."
Hakikisha umechagua mtandao sahihi na umetuma kwenye anuani sahihi ya waleti.Ukichagua mtandao usio sahihi, fedha zako hazitorudishwa.